Pekua orodha bora yenye zaidi ya michezo 200,000 kwenye simu na kompyuta upate mchezo unaokufaa
Pata pointi za Google Play1 unazoweza kutumia kununua michezo na kupata manufaa ya kipekee ukiwa mwanachama wa mpango wa Google Play Points
Pata taarifa kuhusu michezo unayopenda na mafanikio yako kwenye michezo katika kichupo kimoja cha Wewe kinachofaa2
Katika zaidi ya michezo 200,000 kwenye simu na kompyuta, kila mtu atapata mchezo unaomfaa kupitia Michezo ya Google Play. Pata mapendekezo na maelezo ya kina kuhusu kila mchezo, ili ujue ni mchezo upi utakaopenda zaidi baada ya huu. Angalia michezo inayopatikana kwenye simu na kompyuta.
Pata zawadi za kiwango cha juu ukitumia Google Play Points, mpango wa zawadi wa Google Play ambapo unaweza kupata pointi na zawadi za kutumia ili kupata mapunguzo na vipengee vilivyo ndani ya mchezo. Kadiri unavyopata pointi zaidi za Google Play, ndivyo utakavyopata zawadi, manufaa na hali ya juu zaidi ya utumiaji. Jiunge sasa1.
Wasifu wako wa Mchezaji upo katika kichupo cha Wewe. Unaweza kubadilisha kwa urahisi kati ya kichupo cha Wewe na Wasifu wa Mchezaji wakati wowote kwa kubofya aikoni ya wasifu kwenye simu. Ukiwa na wasifu mmoja kwenye simu na kompyuta, unaweza kufuatilia kwa urahisi takwimu, mifululizo, mafanikio na hatua ulizopiga kwenye michezo unayocheza. Ushindi na mafanikio yote, furahia yote katika sehemu moja.
Kisaidizi cha Michezo ya Google Play kwenye Gemini Live ni kisaidizi kipya cha michezo kinachokuwezesha ufikie takwimu zako, mafanikio na vidokezo kwa urahisi bila kuondoka kwenye mchezo wako. Unaweza pia kupata mwongozo wa mazungumzo katika muda halisi kutoka Gemini Live unapocheza. Kisaidizi kinapatikana tu unapocheza michezo uliyopakua kutoka kwenye Google Play na kinakuja hivi karibuni katika simu.
Cheza bila wasiwasi kwenye simu na kompyuta yako, ukiwa na usalama na ulinzi kutoka Google. Google Play hutekeleza ukaguzi wa usalama zaidi ya mara 10,000 katika kila mchezo tunaotoa ili kusaidia kulinda data na vifaa vyako.