Jinsi Google inavyotumia vidakuzi

Ukurasa huu unafafanua madhumuni ambayo Google hutumia vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana. Unaelezea pia jinsi Google na washirika wetu hutumia vidakuzi katika utangazaji.

Vidakuzi ni vifungu vidogo vya maandishi yanayotumwa kwenye kivinjari chako na tovuti unayotembelea. Husaidia tovuti hiyo kukumbuka maelezo kuhusu ulikotembelea, hali inayoweza kurahisisha shughuli ya kutembelea tovuti tena na kufanya tovuti ikufae zaidi. Teknolojia nyingine zinazofanana, ikiwa ni pamoja na vitambulishi mahususi vinavyotumiwa kutambua programu au kifaa, lebo za pikseli na hifadhi ya mfumo, zinaweza kutekeleza jukumu sawa. Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana, jinsi zinavyofafanuliwa kote kwenye ukurasa huu zinaweza kutumiwa kwa madhumuni yaliyofafanuliwa hapa chini.

Angalia Sera ya Faragha ili upate maelezo kuhusu jinsi tunavyolinda faragha yako katika utumiaji wetu wa vidakuzi na maelezo mengine.

Madhumuni ya vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana ambazo hutumiwa na Google

Huenda Google ikahifadhi au kutumia baadhi ya vidakuzi au vidakuzi vyote au teknolojia nyingine zinazofanana katika kivinjari, programu au kifaa chako kwa madhumuni yaliyofafanuliwa hapa chini. Ili udhibiti jinsi vidakuzi vinavyotumiwa, ikiwa ni pamoja na kukataa matumizi ya vidakuzi kwa madhumuni fulani, unaweza kutembelea g.co/privacytools. Unaweza pia kudhibiti vidakuzi kwenye kivinjari chako (ingawa huenda vivinjari vya vifaa vya mkononi visiwe na uonekanaji huu). Baadhi ya teknolojia hizi zinaweza kudhibitiwa katika mipangilio ya kifaa chako au katika mipangilio ya programu.

Utendaji

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana ambazo hutumiwa kwa madhumuni ya utendaji hukuruhusu ufikie vipengele vya msingi vya huduma. Vidakuzi hivi hutumiwa ili kutoa na kudumisha huduma za Google. Mambo yanayochukuliwa kuwa ya msingi kwa huduma ni pamoja na kukumbuka chaguo na mapendeleo, kama vile lugha unayochagua; kuhifadhi maelezo yanayohusiana na kipindi chako, kama vile maudhui ya kikapu chako cha ununuzi; kuwasha vipengele au kutekeleza majukumu uliyoomba; na uboreshaji wa bidhaa unaosaidia kudumisha na kuimarisha huduma hiyo.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana hutumiwa kudumisha mapendeleo yako. Kwa mfano, watu wengi wanaotumia huduma za Google wana kidakuzi kinachoitwa ‘NID’ au ‘_Secure-ENID’ katika vivinjari vyao, kulingana na chaguo zao za vidakuzi. Vidakuzi hivi hutumiwa kukumbuka mapendeleo yako na maelezo mengine, kama vile lugha unayopendelea, idadi ya matokeo ambayo ungependa yaonyeshwe kwenye ukurasa wa matokeo ya utafutaji (kwa mfano, 10 au 20) na iwapo ungependa kuwasha kichujio cha Utafutaji Salama kwenye Google. Muda wa kila kidakuzi cha ‘NID’ huisha baada ya miezi 6 kuanzia kinapotumiwa mara ya mwisho na mtumiaji. Kidakuzi cha ‘_Secure-ENID’ hudumu kwa miezi 13. Vidakuzi vinavyoitwa ‘VISITOR_INFO1_LIVE’ na ‘__Secure-YEC’ hufanya kazi sawa kwenye YouTube na pia hutumiwa kutambua na kutatua matatizo ya huduma. Vidakuzi hivi hudumu kwa miezi 6 na miezi 13, mtawalia.

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana hutumiwa kudumisha na kuboresha hali yako ya utumiaji katika kipindi mahususi. Kwa mfano, YouTube hutumia kidakuzi cha ‘PREF’ kuhifadhi maelezo kama vile mipangilio ya ukurasa unaopendelea na mapendeleo ya uchezaji kama vile chaguo mahususi za kucheza kiotomatiki, kuchanganya maudhui na ukubwa wa kichezaji. Kwenye YouTube Music, mapendeleo haya yanajumuisha kiwango cha sauti, hali ya kujirudia na kucheza kiotomatiki. Muda wa kidakuzi hiki huisha miezi 8 baada ya mara ya mwisho kutumiwa. Kidakuzi cha ‘pm_sess’ pia husaidia kudumisha kipindi chako cha kivinjari na huduma kwa dakika 30.

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana zinaweza pia kutumiwa kuboresha utendaji wa huduma za Google. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘CGIC’ huboresha utoaji wa matokeo ya utafutaji kwa kukamilisha kiotomatiki hoja za utafutaji kulingana na maudhui ambayo mtumiaji aliweka awali. Kidakuzi hiki hudumu kwa miezi 6.

Google hutumia kidakuzi cha ‘SOCS’, ambacho hudumu kwa miezi 13, kuhifadhi hali ya mtumiaji kuhusu chaguo zake za vidakuzi.

Usalama

Google hutumia vidakuzi na teknolojia zinazofanana kwa madhumuni ya usalama ili kukulinda kadiri unavyotumia huduma kwa kuthibitisha watumiaji, kukulinda dhidi ya taka, ulaghai na matumizi mabaya na kufuatilia hitilafu.

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana ambazo hutumiwa kuthibitisha watumiaji husaidia kuhakikisha kuwa mmiliki halisi wa akaunti ndiye tu anayeweza kufikia akaunti hiyo. Kwa mfano, vidakuzi vinavyoitwa ‘SID’ na ‘HSID’ huwa na rekodi zilizotiwa saini dijitali na zilizosimbwa kwa njia fiche, za kitambulisho cha Akaunti ya Google ya mtumiaji na muda wa hivi majuzi zaidi wa kuingia katika akaunti. Mseto wa vidakuzi hivi huruhusu Google kuzuia aina nyingi za mashambulizi, kama vile majaribio ya kuiba maudhui ya fomu zinazotumwa kwenye huduma za Google. Vidakuzi hivi hudumu kwa miaka 2.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana hutumiwa kutambua taka, ulaghai na matumizi mabaya. Kwa mfano, vidakuzi vya ‘pm_sess’ na ‘YSC’ huhakikisha kuwa maombi katika kipindi cha kuvinjari yamefanywa na mtumiaji wala si na tovuti nyingine. Vidakuzi hivi huzuia tovuti hasidi zisichukue hatua kwa niaba ya mtumiaji bila yeye kufahamu. Kidakuzi cha ‘pm_sess’ hudumu kwa dakika 30, na kidakuzi cha ‘YSC’ hudumu kwa kipindi ambacho mtumiaji anavinjari. Vidakuzi vya ‘__Secure-YEC’ na ‘AEC’ hutumiwa kutambua taka, ulaghai na matumizi mabaya ili kusaidia kuhakikisha kuwa watangazaji hawatozwi kimakosa kwa ajili ya maonyesho au shughuli za ulaghai au zisizo sahihi au kwa mitagusano na matangazo; na kuwa watayarishi wa YouTube walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube wamelipwa kwa njia ya haki. Kidakuzi cha ‘AEC’ hudumu kwa miezi 6 na kidakuzi cha ‘__Secure-YEC’ hudumu kwa miezi 13.

Takwimu

Google hutumia vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana kwa madhumuni ya takwimu na kuelewa jinsi unavyotumia huduma husika. Vidakuzi hivi na teknolojia nyingine zinazofanana husaidia kukusanya data inayoturuhusu kupima kushirikishwa kwa hadhira na takwimu za tovuti. Hatua hii husaidia kuelewa jinsi huduma inavyotumiwa na kuboresha maudhui, ubora na vipengele vyake, huku ikituruhusu pia kubuni na kuboresha huduma mpya.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana husaidia tovuti na programu kuelewa jinsi wageni wanavyotumia huduma zake. Kwa mfano, Google Analytics hutumia seti ya vidakuzi kukusanya maelezo kwa niaba ya biashara ambazo hutumia huduma ya Google Analytics na kuripoti takwimu za matumizi ya tovuti kwa biashara hizo bila kuwatambulisha wageni mahususi. ‘_ga’, ndicho kidakuzi kikuu kinachotumiwa na Google Analytics na huwezesha huduma kutofautisha mgeni mmoja na mwingine na hudumu kwa miaka 2. Tovuti yoyote inayotekeleza Google Analytics, ikiwa ni pamoja na huduma za Google, hutumia kidakuzi cha ‘_ga’. Kila kidakuzi cha ‘_ga’ ni mahususi kwenye kipengee mahususi, kwa hivyo hakiwezi kutumiwa kumfuatilia mtumiaji au kivinjari fulani kwenye tovuti zisizohusiana.

Huduma za Google pia hutumia vidakuzi vya ‘NID’ na ‘_Secure-ENID’ kwenye huduma ya Tafuta na Google na vidakuzi vya ‘VISITOR_INFO1_LIVE’ na ‘__Secure-YEC’ kwenye YouTube, kwa ajili ya takwimu. Programu za Google za vifaa vya mkononi zinaweza pia kutumia vitambulishi mahususi, kama vile ‘Kitambulisho cha Matumizi ya Google’, kwa ajili ya takwimu.

Matangazo

Google hutumia vidakuzi kwa madhumuni ya utangazaji, ikiwa ni pamoja na kuonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo, kuonyesha na kutekeleza matangazo na kuyawekea mapendeleo (kulingana na mipangilio yako katika myadcenter.google.com na adssettings.google.com/partnerads). Vidakuzi hivi hutumiwa kwa madhumuni ya kudhibiti mara ambazo tangazo huonyeshwa kwa mtumiaji, kupuuza matangazo ambayo umechagua kuacha kuona na kuwasilisha na kupima ufanisi wa matangazo.

Kidakuzi cha ‘NID’ hutumiwa kuonyesha matangazo ya Google katika huduma za Google kwa watumiaji walioondoka katika akaunti, huku vidakuzi vya ‘IDE’ na ‘id’ hutumiwa kuonyesha matangazo ya Google kwenye tovuti zisizo za Google. Vitambulisho vya utangazaji kwenye vifaa vya mkononi, kama vile Kitambulisho cha Matangazo kwenye Android (AdID), hutumiwa kwa madhumuni sawa kwenye programu za vifaa vya mkononi, kulingana na mipangilio ya kifaa chako. Iwapo umewasha matangazo yaliyowekewa mapendeleo, kidakuzi cha ‘IDE’ hutumiwa kuweka mapendeleo kwenye matangazo unayoyaona. Iwapo umezima matangazo yaliyowekewa mapendeleo, kidakuzi cha ‘id’ hutumiwa kukumbuka mapendeleo haya ili usione matangazo yaliyowekewa mapendeleo. Muda wa kidakuzi cha ‘NID’ huisha miezi 6 kuanzia kinapotumiwa mara ya mwisho na mtumiaji. Vidakuzi vya ‘IDE’ na ‘id’ hudumu kwa miezi 13 kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA), Uswizi na Uingereza (UK) na hudumu kwa miezi 24 kwingineko.

Kulingana na mipangilio yako ya matangazo, huduma nyingine za Google kama vile YouTube zinaweza pia kutumia vidakuzi na teknolojia hizi na nyingine, kama vile kidakuzi cha ‘VISITOR_INFO1_LIVE’, katika utangazaji.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana ambazo hutumiwa katika utangazaji ni za watumiaji wanaoingia katika akaunti ili kutumia huduma za Google. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘DSID’ hutumiwa kutambua mtumiaji aliyeingia katika akaunti kwenye tovuti zisizo za Google ili kufuata ipasavyo mipangilio ya kuweka mapendeleo ya matangazo anayoona mtumiaji. Kidakuzi cha ‘DSID’ hudumu kwa wiki 2.

Kupitia mfumo wa utangazaji wa Google, biashara zinaweza kutangaza kwenye huduma za Google na pia kwenye tovuti zisizo za Google. Baadhi ya vidakuzi huruhusu Google kuonyesha matangazo kwenye tovuti za wengine na huwekwa kwenye vikoa vya tovuti unazotembelea. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘_gads’ huwezesha tovuti kuonyesha matangazo ya Google. Vidakuzi vinavyoanza kwa ‘_gac_’ hutoka kwenye Google Analytics na hutumiwa na watangazaji kupima shughuli za watumiaji na utendaji wa kampeni zao za utangazaji. Vidakuzi vya ‘_gads’ hudumu kwa miezi 13 na vidakuzi vya ‘_gac_’ hudumu kwa siku 90.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana hutumiwa kupima utendaji wa matangazo na kampeni na asilimia za walioshawishika kutokana na matangazo ya Google kwenye tovuti unayotembelea. Kwa mfano, vidakuzi vinavyoanza kwa ‘_gcl_’ hutumiwa kimsingi kuwasaidia watangazaji kubaini mara ambazo watumiaji wanaobofya matangazo yao hushawishika kuchukua hatua kwenye tovuti yao, kama vile kufanya ununuzi. Vidakuzi vinavyotumiwa kupima asilimia za walioshawishika havitumiwi kuweka mapendeleo kwenye matangazo. Vidakuzi vya ‘_gcl_’ hudumu kwa siku 90. Teknolojia nyingine zinazofanana kama vile Kitambulisho cha Matangazo kwenye vifaa vya Android zinaweza pia kutumiwa kupima utendaji wa tangazo na kampeni. Unaweza kudhibiti mipangilio ya Kitambulisho chako cha Tangazo kwenye kifaa chako cha Android.

Angalia maelezo zaidi kuhusu vidakuzi vinavyotumiwa kwa utangazaji hapa.

Kuweka Mapendeleo

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana hutumiwa kwa madhumuni ya kuonyesha maudhui yaliyowekewa mapendeleo. Vidakuzi hivi husaidia kuboresha hali yako ya utumiaji kwa kuweka mapendeleo kwenye maudhui na vipengele, kulingana na mipangilio yako katika g.co/privacytools au mipangilio kwenye kifaa na programu yako.

Vipengele na maudhui ambayo yamewekewa mapendeleo hujumuisha mambo kama vile matokeo na mapendekezo yanayofaa zaidi, ukurasa wa kwanza wa YouTube uliowekewa mapendeleo na matangazo yanayolenga mambo yanayokuvutia. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘VISITOR_INFO1_LIVE’ kinaweza kuruhusu mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo kwenye YouTube kulingana na utazamaji na utafutaji wa awali. Na kidakuzi cha ‘NID’ huwezesha vipengele vilivyowekewa mapendeleo vya kukamilisha kiotomatiki katika huduma ya Tafuta unapoandika hoja za utafutaji. Muda wa vidakuzi hivi huisha miezi 6 baada ya mara ya mwisho kutumiwa.

Kidakuzi kingine, ‘UULE’, hutuma taarifa za eneo mahususi kutoka kwenye kivinjari chako kwenda kwenye seva za Google ili Google iweze kukuonyesha matokeo yanayofaa mahali uliko. Matumizi ya kidakuzi hiki yanategemea mipangilio ya kivinjari chako na iwapo umechagua kuwasha mipangilio ya mahali kwenye kivinjari chako. Kidakuzi cha ‘UULE’ hudumu kwa hadi saa 6.

Hata ukikataa vidakuzi na teknolojia nyingine zinazofanana ambazo hutumiwa kuweka mapendeleo, maudhui ambayo hayajawekewa mapendeleo na vipengele unavyoona bado vinaweza kuathiriwa na vigezo vya kimuktadha, kama vile eneo uliko, lugha, aina ya kifaa, au maudhui ambayo unatazama sasa.

Kudhibiti vidakuzi katika kivinjari chako

Vivinjari vingi hukuruhusu udhibiti jinsi vidakuzi huwekwa na kutumiwa unapovinjari na kufuta data ya kuvinjari na vidakuzi. Pia, kivinjari chako kinaweza kuwa na mipangilio inayokuruhusu udhibiti vidakuzi kulingana na tovuti. Kwa mfano, mipangilio ya Google Chrome katika chrome://settings/cookies hukuruhusu ufute vidakuzi vilivyopo, uruhusu au uzuie vidakuzi vyote na uweke mapendeleo ya vidakuzi kwenye tovuti. Google Chrome pia ina hali fiche, ambayo hufuta historia yako ya kuvinjari na huondoa vidakuzi kwenye Madirisha fiche katika kifaa chako baada ya kufunga Madirisha yako yote fiche.

Kudhibiti teknolojia nyingine zinazofanana katika programu na vifaa vyako

Programu na vifaa vingi vya mkononi hukuruhusu udhibiti jinsi teknolojia nyingine zinazofanana, kama vile vitambulishi mahususi vinavyotumiwa kutambua programu au kifaa, huwekwa na kutumiwa. Kwa mfano, Kitambulisho cha Matangazo kwenye vifaa vya Android au Kitambulisho cha Matangazo kwenye Apple vinaweza kudhibitiwa kwenye mipangilio ya kifaa chako, huku vitambulishi mahususi vya programu vikiweza kudhibitiwa kwa kawaida katika mipangilio ya programu.

Programu za Google
Menyu kuu