Sababu zetu za kuuza matangazo,
badala ya matokeo ya utafutaji.

Katika ulimwengu ambao inaonekana kama kwamba kila kitu kinauzwa, kwa nini watangazaji hawawezi kununua nafasi bora katika matokeo yetu ya utafutaji?

Jibu ni rahisi. Tunaamini kuwa unapaswa kuamini matokeo unayopata unapotumia Google. Tangu mwanzo, lengo letu kuu katika utafutaji limekuwa kutoa majibu na matokeo yanayowafaa watumiaji wetu zaidi.

Matokeo ya Google huzingatia wanaotembelea ukurasa wa wavuti pamoja na jinsi ambavyo maudhui yanayopatikana kwenye ukurasa husika yanalingana na utafutaji wako. Matokeo yetu huonyesha yale ambayo jumuia ya mtandaoni inaamini ni muhimu, si yale sisi au washirika wetu tunafikiri unapaswa kuona.

Na ingawa tunaamini matangazo husika yanaweza kusaidia kwa njia sawa na matokeo halisi ya utafutaji, hatutaki mtu yetote achanganyikiwe kuhusu mambo haya mawili.

Kila tangazo kwenye Google limewekewa alama iliyo wazi na limetengwa kutoka matokeo halisi ya utafutaji. Ingawa watangazaji wanaweza kulipa zaidi ili matangazo yao yaonyeshwe kwenye nafasi za juu katika sehemu ya matangazo, hakuna anayeweza kununua nafasi bora katika matokeo ya utafutaji. Vile vile, matangazo huonyeshwa tu iwapo yanahusiana na hoja za utafutaji ulizoandika. Hiyo ina maana kuwa utaona matangazo ambayo ni muhimu pekee.

Baadhi ya huduma za mtandaoni haziamini kuwa kubainisha tofauti kati ya matokeo ya utafutaji na matangazo ni jambo muhimu.

Sisi tunaamini.